Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile aliyesimama akiongea na wanafunzi wa Uuguzi na Ukunga pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kulia akipata maelekezo kuhusu uuguzi na ukunga kutoka kwa mfanyakazi wa Chama cha Uuguzi na Ukunga Bw. Stephano Simba kushoto alipotembelea banda lao wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kulia akikata utepe baadhi ya vitabu kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa Ukunga salama wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bw. Juma Sweda.
Mkurugenzi wa mradi wa Ukunga salama Dkt. Julius Masanika akiongea na wanafunzi wa Uuguzi na  Ukunga pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Bukumbi Bi. Rose Julius ambaye anafadhiliwa na mradi huo mahitaji yake ikiwamo pamoja na ada wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi .
Mkuu wa Chuo Cha Uuguzi na ukunga SCIMVE Bw. Yohana Ngwandu akiongea na wanafunzi wa Uuguzi na Ukunga pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi
Wanafunzi wa Uuguzi na Ukunga pamoja wakimsikiliza kwa amkini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi
Baadhi ya Wasanii wa Kikundi cha sanaa Cha wakiigiza mama mjamzito anaelekea kituo cha kutolea huduma ya afya mapema kwa ajili ya kujifungua salama wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama uliofanyika leo jijini Mwanza katika chuo cha wauguzi na wakunga Bukumbi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akikabidhi matunda kwa baadhi ya wazee alipotembelea kambi ya wazee Bukumbi jijini mwanza.
Picha na WAMJW-MWANZA
………………….
NA WAMJW-MWANZA
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa wadau wa sekta ya afya na watoa huduma za afya hasa wauguzi na wakunga wanatakiwa kujikita zaidi kwenye kuokoa na kuboresha afya ya mama mjamzito na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama (More and Better Midwives) uliofanyika leo katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga Bukumbi kilichopo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
“Sisi sote tunafahamu umuhimu wa wauguzi na wakunga katika kuimarisha afya ya mama na mtoto hivyo Serikali ya awamu ya tano tumejipanga kuhakikisha kuwa tunapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya mama na mtoto” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inafahamu kuna changamoto ya upungufu wa watumishi katika kada mbalimbali za afya pamoja na nyinginezo na wanaendelea kuzifanyia kazi ikiwa kutoa kipaumbele cha ajira za wauguzi na wakunga.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amewaonya wakunga na wauguzi wenye tabia ya kutumia lugha chafu kwa wagonjwa pamoja na kuacha vitendo vya kuwaomba rushwa kwani fani hiyo inaendeshwa kwa taaluma na maadili.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Misungwi Bw. Juma Sweda amesema kuwa wananchi wa Wilaya hiyo wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika kukata bima za afya kwani husaidia kuokoa gharama nyingi pindi wanapopata maradhi na mpaka hivi sasa wananchi wenye bima ta afya inakadiriwa ni 9100.
Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Ukunga Salama nchini Dkt. Julius Masanika amesema kuwa mradi huo utafadhili wanafunzi wa kanda ya ziwa na kanda ya magharibi wanaojiunga na vyuo vya Uuguzi na Ukunga wasio na uwezo kwa kuwalipia ada pamoja na mahitaji mengine.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Uuguzi na Ukunga katika Chuo cha Bukumbi ambaye anafadhiliwa na mradi huo Rose Julius amesema kuwa anawasihi wanafunzi wafanye bidii kwenye masomo ya sayansi na hatimae wachukue fani ya uuguzi na ukunga katika kukabiliana na changamoto za vifo vitokanavyo na uzazi.
Mbali na ufunguzi huo wa mradi wa Ukunga salama unaojulikana kama “More and Better Midwives”  ambao umeshirikisha taasisi isiyo ya Kiserikali JHPIEGO ,wawakilishi kutoka Chama cha wakungwa  Canada(CMA) na Chama cha wakungwa Tanzania TAMA pia alitembelea Zahanati ya Kambi ya wazee Bukumbi,Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure ili kujua hali ya upatikanaji wa dawa .
SHARE
Previous articleMESSI AFIKISHA MABAO 100 BARANI ULAY
Next article