Kesi inayomkabili Msanii maarufu wa kike wa fani ya uigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’
Ikiwa ni na kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii maarufu wa kiume wa fani hiyo, Steven Kanumba leo imeanza kusikilizwa.

Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akidaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu ambapo tukio hilo lilitokea April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.

Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya Jaji Samweli Manyika ambapo imeongozwa na Wakili wa Serikali Faraja George na aliileza Mahakama kwa leo wana Shadi mmoja ambaye ni Mdogo wa Marehemu Steven Kanumba.

Wakili wa serikali alimuuliza Shahidi anaitwa nani na aeleze Mahakama nini kilitokea siku ya tukio hilo .

Shahidi aliieleza Mahakama anaitwa Seth Bosco anaishi Kimara ila wakati tukio hilo linatokea alikuwa anaishi Sinza na Marehemu Kaka yake.

Aliieleza Mahakama siku ya tukio Lulu alikuja kwenye nyumba waliyokuwa wanaishi na baadae Marehemu Kanumba alitoka na taulo kwenda kumpokea nje kisha wakaingia wote ndani.

Amesema baada ya muda mfupi alisikia kama sauti ya ugomvi kwenye koldo Marehemu Kanumba akisema kwanini unaongea na Boyfriend wako mbele yangu kisha ugomvi ukaendelea kisha wakavutana hadi ndani.

Shahidi ameeleza Mahakama wawili hao waliingia ndani na kujifungia lakini bado kelele za kugombana ziliendelea kusikika na baada ya muda alisikia Lulu akipiga kelele na alipoingia ndani alimkuta alama ya kichwa ukutani na Kanumba chini kaegemea ukutani akiwa kapoteza fahamu.

Ameeleza baada ya hapo walimchukua na kumpeleka Hospital ambapo baada ya hapo alikuwa waliambiwa amesha fariki na baada ya tukio hilo hakuweza kumuona Lulu tena.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho na jumatatu kuhakikisha ushahidi unamalizika wote.