Lionel Messi akifumua shuti kuifungia Barcelona kufikisha mabao 100 kwenye michuano ya Ulaya jana Uwanja wa Camo Nou PICHA ZAIDI ANGALIA HAPA

MABAO YA MESSI ULAYA

97 Ligi ya Mabingwa
3   Super Cup 
11 Penalti
82 Mguu wa kushoto
14 Mguu wa kulia 
4   Kichwa 
16 Kutoka nje ya boksi 
5   Mipira ya adhabu ya moja kwa moja 
 
MSHAMBULIAJI Muargentina, Lionel Messi jana amefikisha mabao 100 katika michuano ya klabu Ulaya.
Hiyo ni baada ya Messi jana kuifungia bao la pili Barcelona dakika ya 61 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Olympiacos kwenye mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Camp Nou, mabao mengine ya Barca yamefungwa na Dimitrios Nikolaou aliyejifunga dakika ya 18 na Lucas Digne dakika ya 64. 
Nikolaou akaifungia bao la kufutia achozi Olympiacos dakika ya 89.
Mapema dakika ya 42, refa Mscotland, William Collum alimtoa kwa kadi nyekundu beki, Gerard Pique baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano.