Meneja Uendeshaji na Huduma Multchoice Tanzania Bw. Ronald Baraka Shelukindo akiwa katika maonesho ya miaka 20 ya Kampuni hiyo tangu kuanziswa kwake nchini Tanzania yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo wateja na wananchi mbalimbali wanatembelea maonesho hayo na kujionea huduma mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na kampuni hiyo.
Meneja wa Chaneli ya Maisha Bongo Magic Afrika Mashariki Barbara Kambogi akiangalia wakati mmoja wa wateja wa kampuni hiyo alipokuwa akirembeshwa uso katika maonesho hayo.
 
Balozi wa DSTV Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa akimhudumia mmoja wa wateja waliotembelea katika maonesho hayo yanayoendelea kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
 
 
Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania Bw. Alfa Mria akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa DSTV Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa katika maonesho hayo.
 
 
Afisa Masoko na Mawasiliano wa Multchoice Tanzania Bi. Shumbana Walwa wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake katika maonesho hayo.
 
 
Baadhi ya wateja wakifuatilia moja ya Tamthilia za Bongo Movie katika maonesho hayo.
 
 
Wanamitindo nao hawako nyuma katika kuonyesha mavazi kwenye maonesho hayo.
 
 
Maonesho ya mashindano ya ligi mbalimbali za mpira wa miguu ikiwemo ligi maarufu ya Uingereza (EPL) pia ni miongozi mwa mambo yanayooneshwa katika maonesho hayo.
 
 
Baadhi ya wateja wakiwa katika eneo la kuchezea watoto kama anavyoonekana mmoja wa watoto akicheza katika eneo hilo.
 
 
Mbunifu wa mavazi Ally Lemtulla katikati ni mmoja wa wabunifu wa mavazi watakaoonyesha ubunifu wa mavazi yao katika maonesho hayo.
 
 
Wateja mbalimbali wa kampuni hiyo wakipata huduma katika maonesho hayo yanayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.