Image result for rayvannyMsanii wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Rayvanny ameachia ngoma mpya ‘Tabia’ ambayo amewachana wasanii wengi kuhusu tabia zao.

Ngoma hiyo ambayo Rayvanny amerap, baadhi ya wasanii waliopitiwa na punch line zake ni Diamond, Nay wa Mitego, Ommy Dimpoz, Young Dee, Shilole, Joh Makini Juma Nature na wengineo kibao. Hapa chini ni baadhi lines hizo.

Ila Juma Nature muda mwingi yupo tungi, Alikiba wa Kariakoo yeye ni shisha na Mirungi/

Diamond akiongea kidogo katukana, Love Boy hupenda wasichana/

Ommy Dimpoz kwa vijembe huyo bwana hachoki, dogo mtoboa siri ni Young Killer Msodoki/

Ukikutana na FA kama hakujui haongei, yuko bize na simu kama Bongo Movie Ray/

Nay wa Mitego yeye ni bifu na kuchonga, utasikia yule mtoto bishoo nitamgonga/

Wanao-act kishua Gosby na Young Dee, wasiogopa wajua mengi Kimbunga na Nash Mc/

Shilole, Shishi mitusi kwa mkupuo, sijui stajini ana sweat maana sizioni nguo/

Nikki wa Pili ha-act kiki-crazy, ila kaka yake Joh anamkopi Jay Z/