Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakicheza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Walipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kukabidhi msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo kwa watoto hao kituoni hapo.
Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Khalid Ismail akipokea moja ya kompyuta kati ya 10 kwa niaba ya wenzake toka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Jacquiline Materu(kulia)Msaada huo uliotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo ya watoto hao kituoni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Jacquiline Materu(wapili kulia)na Meneja biashara kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Grace Lyon(kulia)wakiwapigia makofi ya kuwapongeza baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam baada ya kuwakabidhi msaada wa kompyuta 10 uliotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo yao kituoni hapo.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Wakiwa wameshikilia kompyuta 10 walizokabidhiwa msaada na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo yao kituoni hapo.
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Simu ya Vodacom leo imekabidhi msaada wa kompyuta 10 katika Kituo cha Child In The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam kwa watoto wanaoelelewa kituoni hapo. Msaada uliotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo yao kituoni hapo.