Ajali mbaya imetokea asubuhi ya leo ikihusisha Gari dogo la abiria (Hiace) iliyokuwa ikitokea Muleba kuelekea mji mdogo wa Katoro wilayani Chato lililogongana na Gari kubwa la mafuta (Semi) nje kidogo ya mji wa Muleba katikakati ya Kyamiolwa na Kasharunga.

Watu 4 wamekufa leo baada ya hiace kuungua katika Kijiji cha Kashenyi wilayani Muleba, Kamanda Augustino Ollomi athibitisha Kamanda Augustino amesema mwendo kasi wa dereva wa gari dogo la abiria ni chanzo cha ajali hiyo. Ingawa Kamanda Olomi hakuwataja waliokufa, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango amesema miongoni mwao ni dereva wa gari dogo, kondakta na abiria watatu. Amesema watu hao walishindwa kujiokoa kutokana na mlango wa gari kubanwa hivyo kushindwa kufunguka.