KESI inayomkabili muigizaji wa kike, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo Ijumaa, Oktoba 20, imeendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo shahidi wa pili upande wa Jamhuri ametoa ushahidi wake. Shahidi huyo aliyekuwa daktari wa familia ya marehemu Steven Kanumba ameeleza kuwa siku ya tukio alifuatwa na mdogo wa Kanumba, Seth Bosco kwenda nyumbani kumpima ambapo alifika na kumpima shinikizo la damu na sukari.

Aidha mpelelezi ACP Ester Zephania kutoka Kituo cha Polisi Oyster Bay ambaye alikwenda kumkamata Lulu na kufanya uchunguzi wa tukio hilo, naye ametoa ushahidi wake. Baada ya ofisa huyo kueleza hatua zote walizozifanya pia ameieleza mahakama kwamba walikuta mchirizi wa rangi nyeusi kwenye ukuta wa chumba cha Kanumba na panga lililokuwa chini ya uvungu wa kitanda