MWANAMITINDO ambaye mara nyingi anapenda kuacha wazi sehemu kubwa ya mwili, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amefunguka kuwa anajutia akifikisha umri wa miaka 50 hajui maisha yake yatakuwaje.

Sanchi aliiambia Star Mix kuwa, mara nyingi watu wanaposti vitu mitandaoni, lakini wanasahau kuna uzee mbeleni hivyo vitu hivyo vitakuja kuleta shida hata kwa wajukuu. “Unajua hata mimi naweka picha mbalimbali, lakini kila nikikumbuka kuna uzee, ninaishiwa pozi kwa sababu watu wengi wanajisahau kuwa kuna kuzeeka, lakini kiukweli mimi uzee unanikosesha amani kabisa,” alisema Sanchi