Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula(kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Miliki katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamed Abdallah kuhusu miradi ya ujenzi wa shirika inayoendelea katika eneo la Kijichi,Temeke. Mhe. Mabula alikuwa akikagua utendajiwa sekta ya ardhi  katika  ziara yake ya siku mbili Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva(kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula(kushoto) katika ofisi za Manispaa ya Temeke kukagua utendaji wa shughuli za sekta ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula (katikati) akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi wa Manispaa ya Temeke mara baada ya kukagua utendaji wa utoaji huduma za sekta hiyo ambapo aliwataka kuongeza juhudi za ukusanyaji wa kodi za pango la ardhi. Kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo la Temeke Mhe. Abdalla Mtolea na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Bw.Abdalla Chaurembo.kulia kwa Mhe.Mabula ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Felix Lyaniva na Meneja NHC Mkoa   Bw.Isaya Mshamba.
 Kamishina Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Bw. Mathew Nhonge akijibu hoja zilizoibuliwa na Madiwani wa kata mbalimbali za Manispaa ya Temeke wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula alipotembelea kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika Manispaa hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bibi. Sofia Mjema akimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula alipomtembelea kukagua utendaji wa  shughuli za sekta ya ardhi wilayani humo.
 Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula(kulia) akiangalia utendaji kazi wa mfumo mpya wa ukusanyaji kodi ya ardhi wakati wa ziara ya siku mbili Jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Hati Msaidizi kutoka Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Brenda Kuringe akijibu swali kutoka kwa  madiwani wa kata mbalimbali za Manispaa ya Ilala wakati wa kikao katika ziara ya  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika Manispaa hiyo.