Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia)akifanya mazungumzo na Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Urusi na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo, Komredi Gennady Zyuganov (wa pili kushoto) alipomtembelea leo ofisini kwake katika maadhimisho ya miaka 100 ya Mapinduzi Makuu ya Urusi. Mheshimiwa Spika yupo nchini Urusi, akishiriki Mkutano wa 137 wa Chama cha Mabunge Duniani unaoendelea leo Jijini St. Petersburg, Urusi

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akivishwa nishani maalum ya maadhimisho ya miaka 100 ya Mapinduzi Makuu ya Urusi na Kiongozi wa Chama cha kikomunisti cha Urusi, Komredi Gennady Zyuganov ambae ni Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Urusi na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo alipomtembelea ofisini kwake. Mheshimiwa Spika yupo nchini humo akishiriki Mkutano wa 137 wa Chama cha Mabunge Duniani.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimkabidhi zawadi Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Urusi na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo Komredi Gennady Zyuganov (katikati) alipomtembelea ofisini kwake. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini huko, Jenerali Mstaafu Wynjones kisamba. Mheshimiwa Spika yupo nchini humo kushiriki mkutano wa 137 wa Chama cha Mabunge Duniani.

PICHA NA OFISI YA BUNGE