Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Ushiriani wa Biashara na Uwekezaji kati ya China na Tanzania likilofanyika Guangzhou China tarehe 16 Oktoba 2017. wakiwa katika picha ya pamoja Katikati ni Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof.  Adolf Mkenda aliyekuwa Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo, kulia kwake ni Adam Kimbisa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki; Katibu Mkuu wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Bw. Juma Alli Juma; Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki, na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Akaro. Kulia kabisa aliyesimama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga.
 Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Makamu Rais wa Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa China ‘CADFUND”. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bwn. Francis Assenga, Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji ,Adolf Nkenda, Makamu Rais na Naibu Mtendaki Mkuu wa CadADFUND, Wang Yong na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja.
 
 Kutoka kushoto ni Michael Kitulizo (Mtendaji Mkuu wa Mema Holdings), Mhe. Mbelwa Kairuki (Balozi wa Tanzania Nchini China  ) Prof. F. Lekule (Mtendaji Mkuu wa International Tanfeeds Ltd), Francis Assenga (Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kilimo -TADB) wakati wa Kongamano la Biashara Viwanda na Uwekezaji kati ya China na Tanzania, mjini Guangzhou China juzi.
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya mazungumzo na Taasisi mbili muhimu za kifedha na kiuchumi nchini china kwa ajili ya upatokanaji wa fedha za uwekezaji mkubwa kwenye miundo mbinu na viwanda nchini Tanzania husuan kwenye Sekta ya Kilimo.

Majadiliano hayo yalifanywa kati ya Ujumbe wa TADB ulioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga alipokutana na Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya China (China Development Bank) Bwn. Chris kwenye Mkutano uliofanyika Shangrila Hotel, Guangzhou China wakati wa Kongamano la Pamoja la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na China.

Pande zote mbili zilikubaliana kuendelea na kuimarisha ushirikiano  utakaowezesha kupatikana kwa fedha kwenye uwekezaji wa miundo mbinu ya kilimo na viwanda vidogo vidogo vya uongezaji thamani kwenye mazao ya kilimo kwa wakulima nchini.

Aidha, TADB pia ilikuwa na majadiliano ya kina na Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa Vhina (China African Development Fund) ambao hufanya uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo na ya kibiashara (Equity investmenta) kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Ujumbe wa ulioongozwa na Makamu Mtendaji wa Rais na Naibu Mtendaji Mkuu wa ‘CADFUND’ Bwn. Wang Yong aliyefuatana na Mkurugenzi Mkuu wa Sekta ya Viwanda, Kilimo, Afya & Uwekezaji Bw. Lei Ma; Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Masoko na Huduma Elekezi Bw. Henry Liu; na Meneja wa Uwekezaji wa Viwanda, Ardhi na Kilimo Bw. Luo Zhongquan.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji (UWEKEZAJI) Prof. Adolf Mkenda. Wengine waliohudhuria ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. FRANCIS Assenga; Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki; na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini China Bw. Lusekelo Gwassa.

Katika mazungimzo hayo, pamoja na mambo mengine CADFUND walikubali kuendelea kutoa fedha kwenye miradi ya kiuchumi na uwekezaji mkubwa kwenye nyanja kuu nne zikiwemo kilimo; viwanda; madini; na miundombinu kama ya maji na umwagiliaji.

Aidha CADFUND na TADB ziliainisha maeneo kadhaa ya ushirikiano kama vile Uhakiki na Usimamizi wa miradi; Utafiti; Ukaguzi; na Ujengaji wa Uwezo.