Baba mzazi wa muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, Mzee Michael Kimemeta, amefunguka juu ya matatizo yanayomkabili binti yake, na kusema kwamba angejua mienendo yake inakoelekea angechukua hatua mapema kudhibiti.

 

Mzee Michael ameyasema hayo leo alipokuwa akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba huenda malezi ambayo alikuwa anayapata na kumuacha huru zaidi kufanya akipendacho, ndio kilichomsababishia mwanaye kukutwa na maswahibu hayo.

 

Kuja kwenye tasnia yake sikuona ajabu pamoja na kwamba sikujua kama angekuja kwenye tasnia hii ya usanii, tungekuwa kama wazungu kuangalia watoto ningegundua mapema, maana dalili zilikuwa zinaonekana tangu zamani, ndio maana nilikuwa namkazania kusoma na siku-‘favour’ sana mambo yake ya sanaa ”, amesema mzee Kimemeta.

Mzee Kimemeta ameendelea kwa kusema kwamba hata tukio la kifo cha Kanumba lilitokea wakati akiwa na umri mdogo, na kuwataka watu kutohukumu na kuviachia vyombo husika vifanye uamuzi wake.

Chanzo: EARadio