Msanii wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha amemshutumu mzazi mwenzie, Madam Flora kwa kumzuia kuonana na mtoto wake.Wawili hao ambao wote ni waimbaji ndoa yao ilishavunjika na Madam Flora kuolewa. Akizungumza na TBC Fm amedai kitu anachokifanya siyo kizuri na amekuwa akifanya jitihada za kuonana mwanaye ila imeshindikana.

 

Kiukweli mtoto sijaonana naye muda, yeye mwenyewe hajataka kunipa mimi mtoto, nimeshafanya jitihada na anajua na hata kama sasa hivi anasikia anajua mtoto ameninyima na kitu anachokifanya siyo kizuri kwa mtoto” amesema Mbasha.

 

Ni muda mrefu, mara mwisho nimeona naye (mtoto) mahakamani, muda mrefu kipindi wanakaribia kufunga harusi. Inaniumiza sana ni mtoto wa kipekee, ni mtoto ambaye nampenda na nimeishi naye kipindi chote tangu mdogo”