Mrembo kutoka Tanzania Julitha Kabete aliyechaguliwa kwenda katika mashindano ya urembo wa dunia, Miss World 2017 kwaajili ya kuiwakilisha taifa kwa mwaka huu ameshafika nchini China.

 

Julitha aliondoka siku ya Oktoba 19, mwaka huu kuelekea nchini humo katika mji wa Sanya, kwaajili ya shindano hilo linalohusisha nchi zipatazo 120 duniani kote. Kilele cha mashindano ya Miss World 2017 yanatarajiwa kufanyika ifikapo Novemba 18 mwaka huu, katika ukumbi wa Sanya City Arena na kituo cha E! na Phoenix TV, ndiyo watakaorusha matangazo hayo mubashara.