Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji wa Wizara, Taasisi na miradi iliyo chini yake kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara, Taasisi na miradi iliyo chini yake (hawapo pichani)
 
Sehemu ya watendaji wa Wizara ya Madini, Taasisi na miradi iliyo chini yake wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo pichani)
 
 
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akifafanua jambo katika kikao hicho.
 
 
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Benjamin Mchwampaka (hayupo pichani) katika kikao hicho.
 
 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mhandisi John Nayopa akitoa ufafanuzi katika kikao hicho.
 
 
Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Benjamin Mchwampaka akielezea sekta ya madini katika kikao hicho.
 
…………..
 
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki leo tarehe 21 Oktoba, 2017 amekutana na watendaji wa Wizara pamoja na Taasisi na Miradi katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto za miradi ya maendeleo. Taasisi na miradi iliyoshiriki ni pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji (TEITI). Kikao hicho pia kilishirikisha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo