Wolper amesema hawezi kuvumilia ujinga wa kunyanyasika na kuteseka kwenye uhusiano na mwanaume kwa kuogopa jamii kumsema vibaya wakati mkosaji akiwa ni mwanaume

“Kila mtu anatakiwa kuwa na maamuzi yanayompa faraja, si kila jambo lazima liwe sawa na mtu mwingine kifikra, kuna baadhi ya wanawake wanajikuta wakinyanyasika kwa kuhofia jamii itawaonaje wakiachana na waume wasaliti, ila kwangu haipo hivyo” amesema