VIDEO Queen Sasha Kasim ‘Sasha’ hivi karibuni amedaiwa kutapeliwa pesa za gari na mpenzi wake (jina linahifadhiwa) ambaye ni mume wa mtu kitendo kilichomsababisha adate na kukimbilia Zanzibar ambapo ameenda kupumzisha mawazo.
Sosi wa habari hii aliye karibu na Sasha alidai kuwa Sasha na mwanaume huyo wamekuwa wapenzi kwa mwaka mmoja na walikuwa wameahidiana mambo makubwa ya kimaendeleo lakini mwanaume huyo amekuwa tapeli kwani hivi karibuni Sasha alinunua gari akalichukua yeye.

Huwezi kuamini alimshauri waliuze alafu atamnunulia lingine, gari hilo lilikuwa ni ractis akamshawishi wauze kisha atamnunulia Mark X ambalo mpaka sasa hajalinunua na pesa ameingia nazo mitini kamuacha Sasha akiwa analia,” alisema Sosi.
Baada ya sosi kuanika hayo Sasha aliendewa hewani na kukiri kutapeliwa na bwana huyo ambapo mpaka sasa hajamnunulia gari lingine na hata hajulikani yuko wapi.

 

Namstahi kwa sababu ni mume wa mtu lakini asipotokea nitamfanyia mbaya kwa kumuanika kwani amenisababishia stress mbaya na amenifanya nisiingie kwenye mahusiano na mtu mwingine yeyote kwani simwamini tena kiukweli,” alisema Sasha.
STORI: HAMIDA HASSAN