Wanamuzi wakongwe Bongo, Mwana FA (kushoto), Ambwene Yessaya (katikati) na Fareed Kubanda (kulia0 wakiwa katika picha ya pamoja.
Ngoma kali ya wakali na legends wa Bongo Fleva nchini Tanzania ambao pia wanatamba nje ya Tanzania, Hamis Mwinjuma, Ambwene Yessaya na Fareed Kubanda inayokwenda kwa jina la “UPO HAPO” inapatikana exclusively kupitia Mkito App ambayo imezinduliwa rasmi hiyo jana na inapatikana kwenye Playstore http://bit.ly/-Mkito-Android-App
Mkito App inakuwezesha kusikiliza na kupakua nyimbo za wasanii wa ndani ya Tanzania na wa Kimataifa BILA KIKOMO katika ladha tofauti kama Afrobeat, Genge, Bongo Flava, Swahili Rap, Fusion, Jazz, Singeli, Taarab, Zouk, Soul, Reggae, muziki wa jadi, Beats, Mashairi na maudhui mengine ya sauti – popote ulipo.
Katika jambo ambalo Mkito wamefanya poa sana ni kuiwezesha App hiyo kucheza nyimbo ambazo umezitunza kwenye simu yako au au kadi ya kumbukumbu na kuhakikisha kuwa mzuka unaendelea popote unapoenda! Ipakue leo ufurahie kile ambacho umekuwa ukikosa.

Jinsi ya kupata Punguzo kupitia Coupon
Pakua Mkito App kwenye simu yako
Jisajili kwa kupitia barua pepe au akaunti ya mtandao wa kijamii
Ongeza salio kwenye akaunti yako ya Mkito (MPesa/Tigo Pesa/Paypal)
Jiunge na kifurushi (Ingiza code “UPOHAPO” unapojiunga upate punguzo la 50%)Furahia muziki bila kikomo popote ulipo
Haya ni baadhi ya matukio katika uzinduzi wa video hiyo ya UPO HAPO uliofanyika Tips Bar Mikocheni.