Rais Magufuli akihutubia.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Oktoba, 2017 amewabeza baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanaowarubuni wananchi kwa kuwaeleza kuwa Mapato ya Taifa yameshuka na uchumi umedorora.Magufuli ameyasema hayo wakati akiwatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick Gold.
“Tulipopeleka hati ya dharula bungeni, wapo wengine waliona hili suala si dharula, walitaka tuendelee kuibiwa hata mpaka mwaka 2020. Waliokuwa wanapinga walikuwa wanayasemea matumbo yao na wala hawataweza kuacha kuzungumza, lakini Watanzania wazalendo waliiunga mkono serikali. Sikushangazwa na waliokuwa wakiongea na ningeshangaa kama wasingeongea kwa sababu ndio uzito wa mawazo yao.Mtu anasema mapato yameshuka huku akijua si kweli kuwa yameshuka. Inatakiwa wawe wanafikishwa Mahakamani ili kuthibitisha kauli zao. Kwenye Serikali ambayo mapato yameshuka, unawezaje kununua ndege sita kwa mpigo, tena mpya? Utabadilishana na dagaa? alihoji Rais Magufuli.Kama hatuna pesa, tunawezaje kutangaza zabuni ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua umeme wa Stieglers Gorge ambao mpaka sasa kampuni zaidi ya 75 zimewasilisha maombi ya kujenga mradi huo?Uchumi ungekuwa umeshuka tungewezaje kununua meli kubwa Ziwa Victoria? Kujenga barabara na kuongeza bajeti ya madawa? Wapuuzeni hao wanaopinga, wana lengo la kutupotosha tunakoelekea,” alisema Rais Magufuli.