Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo ya uharibifu wa tuta la mto mkondoa mjini Kilosa kutoka kwa Meja. Yenu Mgugule, kulia kwa Waziri ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. jen. Mbazi Msuya.

Muonekano wa tuta la mto mkondoa mjini Kilosa ambalo limeanza kupasuka kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanywa kando ya mto huo na baadhi ya wananchi wa mji huo. Tuta hilo lenye urefu wa km 4.36 na kimo cha wastani wa mita 5 lilijengwa na serikali baada ya tuta la awali kuharibika kutokana na mafuriko yaliyotokea mwaka 2010.

Sehemu ya tuta la mto mkondoa mjini Kilosa ambayo nyasi zinazozunguka tuta hilo kuzuia maji wakati wa mafuriko zimechomwa moto na baadhi ya wananchi wa mjini humo. Nyasi hizo zilipandwa na Jeshi la Wananchi Tanzania waliokuwa na jukumu la urejeshaji wa tuta hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na wananchi wa mjini Kilosa (hawapo pichani), ambapo alielekeza Halmashauri hiyo kuw na mpango mkakati wa kulilinda tuta hilo pamoja na kuwaonya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa tuta hilo.

Baadhi ya Wananchi wa mjini Kilosa wakinyoosha mikono kuashiria kuunga mkono magizo juu ya kulilinda tuta la mto mkondoa kwa kutofanya shughuli za kibinadamu zilizokuwa zinaendelea pembenzoni mwa mto na tuta. Maagizo hayo yalitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).

Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu