Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amehaidi kukabiliana vilivyo na Korea ya Kaskazini baada ya matokeo ya kwanza kuonesha kuwa alipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi siku ya jumapili.

Bw.Abe alikuwa ameitisha uchaguzi wa mapema kwa ahadi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili Japan likiwemo tishio kutoka Korea ya Kaskazini.

Pia vyombo vya habari vinaripoti kuwa Muungano wa Bwana Abe umeshinda theluthi mbili ya viti vya bunge.

Hii inampa Bw. Abe nafasi ya kuifanyia mabadiliko katiba ya baada ya vita vya pili vya dunia.

Awali waziri mkuu alikuwa ametoa wito wa kutaka jeshi la nchi lifanyiwe mabadiliko, hatua yenye utata ambayo inasema kuwa inahitajika kuboresha ulinzi wa jeshi la Japan.

Akizungumza baada ya kutolewa matokeo ya kwaza Bw. Abe alisema: “Jinsi nilivyoahidi lengo langu kubwa ni kuikabili Korea Kaskazini.