Mwanamume mmoja kutokea nchini Scotland ambaye alishtakiwa kwa upotovu wa maadili mjini Dubai amesamehewa baada ya mfalme wa mji huo kuingilia kati.

Jamie Harron, 27, kutoka Stirling alikuwa amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela kwa kumgusa kiunoni mwanamume mwengine wakiwa kwenye baa.

Kundi linalomuakilisha Bw. Harron huko Dubai linasema kuwa alisamehewa na Sheikh Mohammed bin Rashid al-Maktoum. Na lilisema kuwa Harron alirejeshewa paspoti yake na yuko huru kuondoka Dubai.