CRISTIANO Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka FIFA la mchezaji bora wa kiume wa mpira wa miguu mwaka 2017 ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na ligi ya mabingwa Ulaya – Champions League.

Ronaldo aliyepata watoto mapacha hivi karibuni alipokea tuzo yake mjini London na aliwashukuru mashabiki wake wa Real Madrid, wachezaji wenzake, kocha na rais wake.

Tuzo hiyo kwa mchezaji bora mwanamke imenyakuliwa na mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona.

Aliwahi pia kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi iliposhinda mashindano ya Euro 2017.

Ronaldo ambaye pia alikumbwa na kashfa ya ukwepaji kulipa kodi amewashinda wachezaji Messi wa Barcelona na Neymar wa PSG