Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuhukumu jela maisha Mkazi wa Dar es Salaam Faraja Said amehukumiwa kwenda jela maisha kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 8.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi Ritha Tarimo amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na kumkuta mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Katika ushahidi uliotolewa na shahidi wa kwanza ambaye ndio mtoto aliyebakwa alieleza namna mshtakiwa huyo alivyombaka na kuonesha kuwa kweli mshtakiwa alifanya kosa hilo.

Ilidaiwa mahakamani hapo Daktari wa hospitali ya Amana alithibitisha kuwa mtoto huyo alibakwa ambapo alipomchukua vipimo waligundu kuwa ameingiliwa kumwili na kukuta michubuko.

Hakimu alimuuliza mshtakiwa kama ana chochote cha kuiambia Mahakama kabla ya kutoa adhabu ambapo alijibu anaomba apunguziwe adhabau ana Mke na watoto wanamtegemea.

Mwendesha mashtaka Anuciantha Leopold alisema hakuna kumbukumbu za makosa ya nyuma ya mshtakiwa hivyo apawe adhabu ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama yake.

Hakimu alimuhukumu kwenda jela maisha.