Ahmadreza Djalali
Mahakama nchini Iran inaaminika kumhukumu kifo daktari mmoja mzaliwa wa Iran aliye na kibali cha kuishi nchini Sweden wakimtuhumu kwa kuifanyia ujasusi Israel.Mkuu wa mashtaka nchini Iran alisema mtu alipatikana na hatia ya kuwapasha habari majasusi wa Israel anuani 30 za wanasayansi wa nyuklia, wawili kati yao waliouawa kwenye mashambulizi ya mabomu mwaka 2010.
Lakini mke wake daktari Ahmadreza Djalali, alisema kwa mume wake alikuwa amekuhukumiwa kwa mashtaka sawa na hayo.
Shirika la kupigania haki za binadamu la Amnety International, lilisema kwa hukumu hiyo ilitolewa baada ya mateso ya kisaikolojia na hukumu isiyo ya haki.Mkuu wa mashtaka huko Tehran Abbs Jafari-Dowlatabadi, aliuambia mkutano wa maafisa wa mahakama kuwa mtu ambaye hakutajwa jina aliwapa majasusi wa Isreal anuani za watu 30 muhimu.
Alisema kuwa anuani hizo ni za wanasayansi wa nyuklia Massoud Ali-Mohammadi na Majid Shahriari, ambao waliuawa kwenye milipuko ya mabomu mjini Tehran mwezi Januari na Novemba mwaka 2010.
Mkuu wa mashtaka alisema kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa hizo kwa Israel ili alipwe pesa na msaada wa kupata kibali cha kuwa mkaazi wa Sweden.
Amnesty international ilisema kuwa Bw. Djalali ambaye ni daktari na muathiri kwenye taasisi ya Karolinska mjini Stockholm, alikuwa kwenye ziara ya kibishara nchini Iran mwezi Aprili mwaka 2016, wakati alikamatwa na maafisa wa ujasusi na kuzuiliwa bila ya kuruhusiwa kukutana na wakili kwa muda wa miezi saba.
Bw. Djalali anasema kuwa wakati akiwa kuzuizini alilazimishwa mara mbili kukiri mbele ya kamera kwa kusoma taarifa zilizokuwa zimeandikwa na wale waliokuwa wakimhoji.
Anasema alikuwa chini ya shinikizo kali kupitia mateso ya kisaskolojia na vitisho vya kumuua na kuwakamata watoto wake ili aweze kukiri kuifanyia ujasusi serikali ya Israel.