Mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zimezinduliwa rasmi leo Jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Chama Cha Riadha Tanzania, wadhamini na waandaaji.

Akizindua mbio hizo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Mh. Dk. Harrison Mwakyembe alisema Kilimanjaro Marathon imejizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa maandalizi yake ni mazuri na kuwataka waandaaji wa mbio nyingine kuiga mfano huu.

“Tunataka kuwaibua kina Felix Simbu wengine na hili linawezekana tu kupitia mbio kubwa kama Kilimanjaro Marathon. Nimefahamishwa kuwa Simbu pia alitokana na mbio hizi kwani aliwahi kushiriki kilometa 21 miaka ya nyuma…sisi kama serikali tutafanya kila linalowezekana kuyafikia malengo haya,” alisema.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Executive Solutions Ltd, Aggrey Marealle akitambulisha meza kuu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 jijini Dar es Salaam.

Alishukuru pia wadhamini wengine ambao ni Tigo-21km, Grand Malt 5km na wale wa meza za maji ambao ni pamoja na First National Bank, Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Simba Cement na KNAUF Gypsum.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis alisema wanajivunia kudhamini mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ambazo zinakuwa kwa kasi kubwa mwaka hadi mwakana hii inawapa moyo na ari ya kuendelea kuwa wadhamini.

Alisema udhamini huu katika mbio za kilometa 42 na 5 kupitia Grand Malt, pamoja na mambo mengine unalenga kuibua vipaji zaidi katika riadha na kuwataka washiriki kujiandaa vizuri. “Inabidi tujiamini zaidi kwani siku moja wimbo wa Taifa wa Tanzania utapigwa katika mbio maarufu duniani,” alisema.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe akitoa hotuba wakati wa uzinduzi rasmi Mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alitoa rai kwa washiriki kuhakikisha wanajiandikisha mapema li kuepuka usumbufu dakika za mwisho na kutoa mfano wa mwaka huu ambapo namba za ushiriki zilikwisha kutokana na watu wengi zaidi kujitokeza. “Tumeshazungumza na waandaaji ili kuwepo na namba za kutosha mwakani,” alisema.

Alisema ujumbe mkuu wa Kilimanjaro Premium Lager kwa mbio za mwakani ni ‘Kunywa kistaarabu usiendeshe ukiwa umekunywa’.”Najua wengi tungependa kufurahia kili zetu baridi baada ya mashindano lakini tunywe kwa ustaarabu,” alisema huku akiongeza kuwa zawadi kwa mshindi wa kilometa 42 ni milioni 4 kwa mwanaume na mwanamke na jumla ya zawadi ni milioni 20 kwa washindi wote.Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis akizungumza kuhusu udhamini wa mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitakazofanyika mwakani Machi 4 mkoani Kilimanjaro. Kushoto Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli na Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe.

Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini,,Henry Kinabo alisema, “Tuna furaha kuwa sehemu ya mbio hizi kwa mara nyingine. Hizi ni mbio ambazo zinawaleta pamoja wanariadha wakubwa na watu kutoka Nyanja mbalimbali kusherekea michezo, kufurahi, kukuza utamaduni, utalii na pia kwa afya bora,” alisema.

Alisema Tigo, inayodhamini mbio za kilometa 21, itatoa jumla ya Milioni 11 kama zawadi huku msindi wa kwanza wa kiume na kike wakijinyakulia milioni 2 kila mmoja wa pili milioni 1 wakati wa tatu watapokwa Tsh 650,00o huku Katia ya 500,000 na 100,000 zikienda kwa washindi kuanzai wan ne hadi wa 10 pamoja za medali za ushiriki kwa kila atakayemaliza mbio.Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli (wa tatu kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko wa TBL anayesimamia kinywaji cha Grand Malt, Warda Kimaro, alisema mbio za Kilometa 5 zinazodhaminiwa na Grand Malt zinakuwa mwaka hadi mwaka na kuwavutia watu wengi zaidi wakiwemo watoto, vijana na watu wazima. “Tumeandaa shughuli mbalimbali za kusisimua kwa ajili ya washiriki kwa hivyo tujiandikishe mapema na tukumbuke kunywa Grand malt kwa kuwa ni kinywaji chenye afya hasa kwa wanariadha,” alisema.

Kilimanjaro Premium Lager Marathon huandaliwa na Wild Frontiers na Deep Blue Media na kuratibiwa na Executive Solutions. Wadau wengine muhimu ni, Chama Cha Riadha Tanzania, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Kilimanjaro Marathon Club, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,vilabu vya jogging na Jeshi la Polisi.Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo (kulia) akizungumzia jinsi kampuni yake ilivyojipanga kutoa huduma mwakani katika mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitazofanyika mwakani machi 4 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.Meneja Masoko wa TBL Group anayesimamia Grand Malt, Warda Kimaro (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais wa Chama Cha Riadha Tanzania, William Kallaghe akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitazofanyika machi 4 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe. na Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis.Pichani juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akizindua rasmi mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 leo Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa TBL Group anayesimamia Grand Malt, Warda Kimaro, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo, Katibu Mkuu wa TOC Filbert Bayi, Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo, Alex Nkenyenge, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis na Makamu wa Rais wa Chama Cha Riadha Tanzania, William Kallaghe.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe katika picha ya pamoja na wadhamini wakuu TBL.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe katika picha ya pamoja na wadhamini wa meza za maji mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitakazofanyika machi 4 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.