Wanafunzi wa Chuo cha Bahari nchini (DMI) wakielea majini huku wameshikilia boya kubwa la kujiokolea lenye uwezo wa kushikwa na watu 12 wakati wa zoezi la kuwafundisha abiria wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni jinsi ya kujiokoa pindi inapotokea dharura ya ajali. Zoezi hilo lililoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kitengo cha Habari na Mawasiliano limefanyika katika kivuko cha Magogoni Kigamboni kwa lengo la kuwapa elimu ya kujiokoa pindi inapotokea dharura watumiaji wa vivuko hivyo.
Mwanafunzi kutoka Chuo cha Bahari nchini (DMI) akiruka kwenye maji huku akitazamwa na baadhi ya abiria wa kivuko cha MV. KAZI wakati wa zoezi la kuwafundisha abiria wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni jinsi ya kujiokoa pindi inapotokea dharura ya ajali. Zoezi hilo lililoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kitengo cha Habari na Mawasiliano limefanyika katika kivuko cha Magogoni Kigamboni kwa lengo la kuwapa elimu ya kujiokoa pindi inapotokea dharura watumiaji wa vivuko hivyo.
Wanafunzi wa Chuo cha Bahari nchini (DMI) wakielea majini huku wameshikilia boya kubwa la kujiokolea lenye uwezo wa kushikwa na watu 12 wakati wa zoezi la kuwafundisha abiria wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni jinsi ya kujiokoa pindi inapotokea dharura ya ajali. Zoezi hilo lililoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kitengo cha Habari na Mawasiliano limefanyika katika kivuko cha Magogoni Kigamboni kwa lengo la kuwapa elimu ya kujiokoa pindi inapotokea dharura watumiaji wa vivuko hivyo.
Abiria waliokua katika kivuko cha MV. MAGOGONI wakimuangalia mmoja wa wazamiaji wakati akirukia kwenye maji katika zoezi la kuwafundisha jinsi ya kuingia majini pindi inapotokea dharura ya ajali katika kivuko. Zoezi hilo lililoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kitengo cha Habari na Mawasiliano limefanyika katika kivuko cha Magogoni Kigamboni kwa lengo la kuwapa elimu ya kujiokoa pindi inapotokea dharura watumiaji wa vivuko hivyo.
Wanafunzi wa Chuo cha Ubaharia (DMI) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza zoezi la kuwafundisha abiria wanaotumia kivuko namna ya kujiokoa pindi inapotokea dharura ya ajali katika maji. Zoezi hilo limeratibiwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wakala wa ufundi na Umeme (TEMESA) na limefanyika katika kivuko cha Magogoni Kigamboni na litaendelea wiki ijayo.
 
 
NA ALFRED MGWENO( TEMESA)
Wanafunzi kutoka chuo cha Bahari nchini (DMI) leo wamefanya zoezi la kufundisha abiria wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni jinsi ya kutumia vifaa vya kujiokolea vilivyomo katika vivuko hivyo pindi inapotokea dharura ya ajali kwenye maji.
Zoezi hilo lililoratibiwa na chuo cha Bahari kwa kushirikiana na kitengo cha Habari na Mawasiliano (TEMESA) limefanyika kivukoni hapo mapema asubuhi likiongozwa na Nahodha Nyamurasa Matage kutoka chuo hicho. Zoezi hilo lilihusisha wanafunzi wa kozi ya PST na lilikua na nia ya kuwaonyesha watumiaji wa kivuko hicho namna ya kujiokoa na pia kujifunza kuwa na utulivu pindi inapotokea dharura ya ajali, moto au kuzimika kwa kivuko.
Akizungumza katika tukio hilo Nahodha Nyamurasa aliwataka watumiaji wa kivuko hicho kuhakikisha wanafuatilia kwa makini zoezi hilo kwani dharura ya ajali inaweza kutokea wakati wowote na mahala popote hivyo abiria wanatakiwa kuwa watulivu pindi inapotokea. Alisema mafunzo hayo yalikua ni sehemu ya masomo yao ya darasani lakini pia elimu tosha kwa watumiaji wa vivuko.
Naye Mkuu wa kivuko Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe akizungumza wakati wa zoezi hilo aliwataka wanafunzi hao kulichukulia kwa umakini zoezi hilo kwani pindi wanapomaliza mafunzo yao wanatumiwa katika vivuko vya TEMESA katika shughuli za uokoaji wa abiria na mali zao na pia kutoa maelekezo ya usalama kwa abiria wa vivuko hivyo, “hili ni zoezi muhimu kwa abiria wetu kulipata na kujifunza namna ya kutumia vifaa vya kujiokolea ambavyo vinakuwepo muda wote katika vivuko vyetu”, alisema..
Dhumuni kubwa la zoezi hilo lilikua ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo hicho na pia kutoa mafunzo kwa abiria wanaotumia kivuko. Zoezi hilo linategemewa kuendelea wiki ijayo katika kivuko hicho.