Mvua inayoendelea kunyesha imelisomba daladala eneo la Mbezi Luisi jijini Dar es Salaam na kudumbukia ndani ya mto. Abiria waliokuwepo ndani ya basi hilo wamefanikiwa kutoka dirishani kunusuru maisha yao.

Barabara katika eneo la daraja la mto mbezi imejaa maji yanayotiririka kuelekea mtoni ambayo ndio yamelisomba gari ya abiria na kutumbukia mtoni. Baadhi ya wakazi wa eneo la mbezi luis wameshindwa kutoka kwenda kazini kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.