Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati.

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati aahirisha uchaguzi kwa baadhi ya maeneo nchini Kenya mpaka siku ya Jumamosi Oktoba 28, 2017 kwa kile kilichoelezwa kuwa baadhi ya maeneo kumekuwa na changamoto mbalimbali kama vile mvua kubwa.

Wafula Chebukati ametaja maeneo ambayo uchaguzi umeiarishwa kuwa ni pamoja na Kisumu Migori, Siaya na Homabay na kuwa katika maeneo hayo uchaguzi utafanyika siku ya Jumamosi, Oktoba 28.

Chebukati amesema wamefikia maamuzi hayo kutokana na maeneo hayo kuwa na changamoto mbalimbali ikiwepo masuala ya usalama pamoja na mvua jambo ambalo limefanya zoezi la kupiga kura kuwa changamoto ka wapigaji kura.