Siku za hivi karibuni, Serikali imetilia mkazo uwezeshaji wa watanzania kumiliki uchumi wao kwa kuyataka makampuni na mashirika kujiorodhesha katika Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE). Makampuni ya simu na mabenki ni miongoni mwa makampuni yaliyoshika kasi katika kujiorodhesha katika Soko la Hisa.Sambamba na hilo, elimu ya uwekezaji katika eneo hili imekuwa na msukumo mdogo tangu ulipoanza kwenye miaka ya 90. Hii inasemekana kuwa pengine ni uchanga na ugeni wa soko letu lakini pia elimu kutowafikia watanzania wengi kwa wingi.Elimu ya masuala ya hisa inaonyesha kujikita zaidi katika maeneo ya mijini hususani jijini Dar Es Salaam ambapo ni sehemu ndogo tu ya idadi ya wananchi wa Tanzania na hivyo kupelekea umuhimu wa Serikali,wataalamu na wadau wa masoko ya mitaji na dhamana kutoa elimu zaidi katika maeneo yote ya nchi kuanzia mijini, vijijini na hata mashuleni ili kujenga uelewa kwa wananchi ili wawe sehemu ya umiliki wa makampuni na mashirika yanayoingia katika soko la hisa.

Kazi hii pia imekuwa ikifanywa na Maendeleo Bank ambayo ndiyo benki inayouza hisa zake sasa kupitia matawi yake, matawi ya CRDB nchi nzima, Uchumi Commercial Bank na kupitia njia ya simu.Maendeleo Bank imekuwa ikitoa elimu ya uwekezaji kupitia semina na mikutano mbalimbali na wananchi wa kada mbalimbali na wafanyabiashara ili kuwapatia uelewa wa kutosha kabla ya kuamua kuwekeza.Baada ya kufanya semina jijini Mwanza wiki iliyopita. Mwisho wa Juma lililopita timu ya viongozi wa Maendeleo Bank walitoa elimu hii Shinyanga Mjini na katika wilaya ya Kahama kwa wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha hawabaki nyuma katika elimu hii muhimu hasa wakati ambapo benki hiyo inauza hisa zake.Maendeleo Bank ilianza kuuza hisa zake Septemba 18 na zitakwenda hadi Novemba 3, 2017. Hisa moja ni shilingi 600 tu na kiwango cha chini ni hisa 100 ambazo ni shilingi 60,000