RAIS John Magufuli amewataka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliyeapishwa leo, Bi. Christine Mndeme ahame kituo na kwenda kufanya kazi kama Mkoa wa Ruvuma huku akimtaka Mkuu wa Mkoa Ruvuma, Mahenge ahamie Mkoa wa Dodoma.Rais ametoa agizo hilo mara baada ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu wa Wizara na Manaibu katibu wakuu aliowateua jana baada ya kufanya mabadiliko machache katika safu yake ya uongozi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mpya, Christine Mdemi atakuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma badala na Dkt. Binilith Mahenge atakwenda Dodoma,” alisema Magufuli.Aidha Rais amewataka Wakuu wa Mikoa wapya, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wapya wakashirikiane na viongozi wengine kwenye maeneo yao kutatua shida za wananchi na kutengeneza mikakati ya kukuza uchumi katikamaeneo yao ya kazi.Kila mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya akaangalie matatizo yaliyopo na kitu gani anaweza kufanya kuongeza uchumi wa eneo lake,” alisisitiza Rai Magufuli.Pia ametoa onyokwa watendaji watakaokula pesa za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini.Nitashangaa kama patakuwepo wanafunzi ambao wapo kwenye orodha ya kupata mikopo na wasipate.
Nimeshaidhinisha bilioni 147 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu na pesa zipo Wizara ya Elimu, mtajua wenyewe mtafanyaje, lakini nitoe onyo, msije mkazitafuna hizo pesa, ziende zikawasaidie watoto wetu wasome, alieleza Rais.