Ndugu Wananchi,
Awali ya yote, Naomba kutoa pole Kwa wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam waliokumbwa na mafuriko na kusababisha usumbufu kwa Baadhi ya Wananchi uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Leo nimepokea taarifa ya Awali kutoka Kwa Wakuu wa Wilaya zote tano zinazounda Mkoa wa Dar es Salaam. ….
Taarifa ya awali inaonyesha kuwepo kwa Uharibufu wa Miundombinu ya Barabara pamoja na Madaraja Kusombwa na maji uku baadhi ya Nyumba nyingi zikiwa zimejaa maji kutokana na changamoto ya miundombinu kutohimili mvua zilizonyesha kwa Muda mrefu. …
Kutokana na sababu hiyo, Nimeona kesho ni vyema niwatembelee wananchi wangu na kwa pamoja tujadili njia bora ya kurejesha miundombinu na hali ya utaratibu wa Makazi ya wananchi katika hali ya kawaida kama ilivyokuwa hapo awali. ……
Mwisho nawaombea Kwa Mungu atupe uvumilivu na kutuepusha na majanga huku tukichukua tahadhari….. Paul Makonda 27/10/2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.