MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye miondoko ya Mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, mambo ya mapenzi ameyaweka kando hivyo watu aliokuwa akitembea nao ‘vi-ben ten’ sasa basi. Akigonga stori na Star Mix, Shilole alisema kuwa, akiyaweka mapenzi mbele mara nyingi hayamzalishii matunda yoyote lakini akikazana katika kazi inamletea mafanikio makubwa.

Jamani kwa usawa huu mtu usipobadilika na kuangalia kitu cha maana ni shida sana, mimi mambo ya mapenzi sijui vi-ben tena sasa hivi yanisubirie kwanza, nifanye kazi zangu ili nipate maendeleo sio mapenzi wanafaidi mashabiki wa Instagram kukuangalia maisha yako,” alisema Shilole. NA IMELDA MTEMA