Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt Julius Mwaiselage
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt Julius Mwaiselage amesema kuwa tatizo la saratani limekuwa likiongezeka siku hadi siku duniani kote na takwimu zinazotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni [WHO] zinaonyesha kwamba kila mwaka wagonjwa wapya milioni 14.1 hugundulika na wagonjwa milioni 8.8 hufariki dunia.

Ugonjwa wa Saratani ya Matiti Unavyoonekana
Ameyasema wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi mapema wa saratani ya matiti inayotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Ameongeza kuwa taasisi yao kwa kushirikiana na Hoteli ya Kunduchi Beach na Hospitali ya Aga Khan ndiyo imeandaa matembezi yatakayoanzia Ocean Road saa 12.30 asubuhi na kuhitimishwa saa 4.00 katika taasisi hiyo ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.