STAA mwenye nyota kali Bongo, Wema Sepetu, amefunguka kuwa hakuna kitu ambacho anakichukia kwenye mwili wake kama tatuu yake ambayo iko shingoni.

Wema alisema alichora tatuu hiyo akiwa bado mdogo na alimwambia mchoraji achore kitu kirefu kishuke shingoni ndipo alipochora kitu kama mjusi.
“Natamani sana kuifuta tatuu yangu hii lakini nasikia vibaya na pia naambiwa kuwa inauma sana kuifuta lakini ningekuwa na uwezo isingekuwepo kabisa,” alisema Wema.

Chanzo Global Publishers