MASTAA wengi wamegubikwa na hofu na huruma nyingi kwa muigizaji mwenzao, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kufuatia kuibuka upya kwa kesi yake ya kuua bila kukusudia ya msanii mwenzake, Steven Kanumba iliyoanza kusikilizwa Oktoba 19, mwaka huu. Mastaa hao ambao wengine nao wameshaonja machungu ya gerezani, wameanika hisia zao na huruma nyingi kwa mwenzao huyo na katika makala haya wanafunguka zaidi;

DAVINA
Huyu naye alishawahi kulala katika Gereza la Segerea kwa kosa la kuvunja kioo cha ofisi ya mzazi mwenziye. Davina anasema kuwa, kesi inayomkabili Lulu ni jambo la kumuomba Mungu ampitishe salama katika kipindi hiki kigumu na ni kipindi cha kuombeana. “Katika hili ni kumuweka Mungu mbele na kumuombea mwenzetu kwa sababu anapita kwenye kipindi kigumu ambacho hakijawahi kuzoeleka hata mara moja.”

Huyu naye alishawahi kulala katika Gereza la Segerea kwa kosa la kuvunja kioo cha ofisi ya mzazi mwenziye. Davina anasema kuwa, kesi inayomkabili Lulu ni jambo la kumuomba Mungu ampitishe salama katika kipindi hiki kigumu na ni kipindi cha kuombeana. “Katika hili ni kumuweka Mungu mbele na kumuombea mwenzetu kwa sababu anapita kwenye kipindi kigumu ambacho hakijawahi kuzoeleka hata mara moja.”

MASOGANGE
Kama ilivyo kwa wengine, huyu naye alishawahi kulala gerezani nchini Afrika Kusini baada ya kudaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo nchini humo. Masogange anamuombea sana Lulu na anaumizwa na wakati alionao sasa hivi kwani ni mgumu mno. “Naelewa jinsi anavyojisikia kwa sasa ila kikubwa tunamuombea kila wakati ili Mungu asimame upande wake, maana ni kipindi kigumu sana kwani hakuna ambaye aliwahi kuifurahia jela.”

 

LULU DIVA
Lulu Diva ni miongoni mwa mastaa waliowahi kukaa mahabusu kwa kosa la kudaiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Diva anasema kuwa, hakuna kubwa la kufanya zaidi ya kumuombea dua ili wakati alionao upite salama. “Jamani ni kipindi kigumu sana anacho mwenzetu wala si la kucheka na kusema kuwa haliwezi kukupata kwa sababu leo yeye kesho wewe.”

WEMA
Naye alishaonja machungu ya gerezani baada ya kudaiwa kuvunja kioo cha gari cha marehemu Kanumba na kupelekwa Segerea. Wema anasema kuwa, anaamini kila binadamu ameumbiwa matatizo ila Mungu atamsaidia Lulu. “Hakuna hata mmoja atakayeona mwenzake yupo kwenye shida kama hiyo akafurahi, mimi nimeonja machungu ya gerezani, namuombea sana Mungu amsimamie katika hili

 

WOLPER “Namuomba sana Mwenyezi Mungu amsaidie katika wakati alionao lakini naamini haya ni mapito atakuwa sawa tu.”

AUNT
Yeye anasema kuwa, anaumizwa na kipindi anachopitia mwenzake lakini kikubwa ni kumuachia Mungu na kumuomba. “Mimi namuombe Mungu tu, aendelee kumsimamia katika kipindi kigumu ambacho anapitia kwa sasa na ninaamini sana Mungu atasimama naye.”

 

KAJALA Ni mmoja wa mastaa ambaye naye alishawahi kuonja adha ya jela ambapo alikaa mwaka mmoja na miezi mitatu baada ya kudaiwa kugushi hati ya nyumba. “Kila kukicha namuomba sana Mungu amsaidie Lulu hili lipite. Nimekaa gerezani na nimeona maisha ya huko yalivyo