Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amemtumia ujumbe Rais wa sasa wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuhusu siku yake ya kuzaliwa ambayo ni leo Oktoba 29.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Jakaya Kikwete ameandika ujumbe huo wa kumtakia heri, huku akizidi kumuombea kwa Mungu, ampatie afya na siha njema.

“Nakutakia kila la kheri Mhe Rais Magufuli unaposherehekea siku yako ya kuzaliwa. Nakutakia afya na siha njema na umri mrefu zaidi”, ameandika Jakaya Kikwete.

Leo Oktoba 29, Rais Magufuli anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo anatimiza miaka 57, tangu alipozaliwa mwaka 1959 huko wilayani Chato mkoani Geita.