Warembo waliokuwa kwenye vita ya maneno, Hamisa Mobeto na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamedaiwa kuwekwa kitimoto ili waache kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii.
Risasi Jumamosi limeelezwa kuwa, kwa nyakati tofauti wawili hao waliwekwa kitimoto na ndugu wa msanii wa Mzazi Mwenzao na kutakiwa waache malumbano hayo mitandaoni kwani hayaleti picha nzuri kwao na ukizingatia kosa limeshafanyika na msanii kukiri hadharani.
“Walichoelezwa tu ni kwamba, waache kutupiana vijembe mitandaoni maana wao sasa hata kama hawatakuwa wake wenza lakini tayari msanii ana damu yake kwa Mobeto. Amekiri kwamba aliteleza na kujikuta ameingia kwenye uhusiano naye hadi kufikia hatua ya kupata mtoto.

Zarinah Hassan.
“Mtoto ameshazaliwa na ni damu ya msanii na mwisho wa siku msanii atalazimika kumpa mahitaji yake kama mwanaye hata kama yeye hataendeleza uhusiano na mama wa mtoto. Zari ni mama wa watoto wake wawili, wamedumu muda mrefu hivyo yeye ataendelea tu kushikilia usukani kama mke,” kilisema chanzo cha ndani kutoka katika familia ya msanii.
Chanzo hicho cha ndani kilizidi kueleza kuwa, wanamshukuru Mungu kwamba mwanamitindo Mobeto na Zari ambaye ni mjasiriamali maarufu, kila mmoja kwa wakati wake ameelewa vizuri somo hilo hivyo kuacha kutupiana manenomaneno katika mitandao ya kijamii.
“Tunashukuru Mungu kwani kila mmoja ameelewa somo. Hawarushiani tena maneno kama ilivyokuwa awali. Zamani ilikuwa hazipiti siku mbili utasikia kuna jipya wame-sababisha lakini sasa hivi kama unafuatilia hata mitandaoni, watu hawawa-zungumzii tena.,” kilisema chanzo hicho
Na MWANDISHI WETU, Risasi Jumamosi