Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewatangazia Wananchi wote wa Dar es Salaam kuwa Daraja la Muda mfupi la Malecela limeanza kutumika leo kuanzia saa kumi jioni baada ya ujenzi kukamilika.

amezungumza hayo leo Baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja ambapo ametoa pole kwa wananchi kwa usumbufu waliopata.

Ili kuhakikisha Daraja hilo linaanza kutumika RC Makonda amesema kuwa hatoondoka kwenye Daraja hilo hadi hapo atakapoona wananchi wanapita na vyombo vya usafiri bila tatizo.

Amepongeza kamati ya Maafa ya Mkoa kwa kukamilisha ujenzi huo ndani ya muda mfupi.

Amesema kuwa Serikali ya Mkoa inaendelea kukarabati miundombinu yote ya Barabara, Umeme,Maji na Madaraja yaliyoharibiwa na Mvua zinazoendelea kunyesha.

Amewataka wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari kwakuwa Mvua bado itaendelea kunyesha kama walivyotangaza wataalamu wa hali ya hewa.

Itakumbukwa kuwa RC Makonda alipofanya ziara ya kukagua miundombinu iliyoharibiwa na Mvua aliagiza kujengwa kwa la muda mfupi baada ya Daraja la Malecela kuharibiwa vibaya na mvua iliyonyesha hivi karibuni.