Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Lughumbi akisalimiana na mwenyeji wake ambaye kwasasa amestaafu kwenye kiti cha ukuu wa Mkoa, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati alipokuwa akiwasili kwenye ofisi za Mkoa huo kwaajili ya makabidhiano ya kuanza shughuli na majukumu ya kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Lughumbi akimkabidhi hati ya pongezi Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akionesha Hati ya pongezi ambayo amepatiwa na Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akiagana na watumishi.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akimkabidhi Mkuu wa Mkoa mambo muhimu ambayo ameyaandika wakati wa hafla ya kukabidhiana ofisi. (PICHA NA MADUKA ONLINE)

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi amewataka watumishi na wakuu wa wilaya Mkoani humo kuwatumikia kikamilifu wananchi wenye matarajio makubwa kwa serikali yao. Mhandisi Lughumbi aliyasema hayo alipozungumza na watumishi na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo katika hafla ya kukabidhiwa ofisi na Mtangulizi wake Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga aliyestaafu nafasi hiyo.

Alisema amefika kwenye Mkoa wa Geita kufanya kazi hivyo watumishi wote wawajibike kuchochea maendeleo kwa kasi ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu.

“Nimeingia katika Mkoa huu kama mlivyonikaribisha mmenikaribisha nimekuja kufanya kazi nimekuja kutumika nimetumwa kuwa mtumishi kwa mwendo tulionao hatuna muda wa kupumzika ni kipindi cha mageuzi lazima tugeuze kitu kigeuzike watu wajue tumegeuza hata wanaofuatilie waone mambo yapo sawa sawa ukione maendeleo yanakimbia ujue uku kulipokuwa kunachelewa vilikuwa vipindi vigumu vya matengenezo”Alisema Lughumbi.

Pia amezungumzia tatizo la uduni wa miundombinu ya elimu na shida ya maji inayoendelea kuwasumbua wananchi wa Geita.

“Wakina mama bado wanandoo kichwani katika Mkoa tupo asilimia hamsini upatikanaji wa maji safi na salama kuna watu wamecheza na fedha ya umma maji hayajaja tangu miaka ya sabini meja jenerali wewe ulikuwa mpole mimi naenda kwenye sait nitakuwa mkali kidogo hasa ambao wanacheza na mali ya umma”Alisisitiza Lughumbi.

Mkuu wa Mkoa mstaafu, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga alisema kwa sasa anakwenda kupumzika na kuwataka wanaobaki kulitumikia taifa wafanye kazi kwa weledi na kasi inayoendana na ile ya Rais Dr John Magufuli.

Mkoa wa Geita ni Kati ya Mikoa ambayo ilianzishwa mwaka 2012,na wakuu wa Miako ambao wamepita hadi sasa ni watatu ,Magalula Said Magalula,Fatuma Mwasa na Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu hivi karibuni na kumpisha ,Mhandisi Robert Lughumbi.