OFISI ya Taifa ya Takwimimu (NBS) imesema kuwa taairifa zilizotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe juu ya takwimu za kushuka kwa uchumi ni za uongo na zimejaa upotoshaji, hivyo zipuuzwe.

Akizungumza na wanahabri leo jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa amesema upotoshaji huo ni wa makusudi na unalenga kuchafua  jitihada zinazofanywa na serikali ya Awamu ya Tano kuinua uchumi zionekane hazina manufaa kwa wananchi.

“Napenda kukanusha kauli ya Zitto Zuberi Kabwe (Mb) kuhusu taarifa zake zinazodai kuwa takwimu za Pato la Taifa zimepikwa.

“Anatakiwa kujua kwamba kazi ya kukokotoa takwimu za pato la Taifa ni ya kitaalamu (kwa nadharia na vitendo) na kazi hii inafuata miongozo inayotolewa na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Takwimu na shirika la fedha Duniani ,“ alisema Masolwa na kuongeza;

 

“Takwimu alizozitumia Zitto za ukuaji wa Pato la Taifa kwenye uchambuzi wake kwa kipindi cha miaka mitano, siyo sahihi  na ukweli ni kwamba  ukuaji wa pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka kuanzia  2013 hadi 2017 ni kama ifuatavyo:

“Takwimu rasmi za kwa mwaka 2013 ni (6.3), 2014 (9.8), 2015 (6.5), 2016 (8.5) na mwaka 2017 ni 7.8 wakati takwimu zisizo rasmi za Zitto Kabwe ni 2013  (7.0) 2014 (8.6) 2015 (5.7) 2016, (6.8) na mwaka 2017 ni 5.7.

 

Kwa mujibu wa mashihisho hayo,  Masolwa alisema Zitto anatakiwa kufahamu kuwa takwimu za robo mwaka hurekebishwa baada ya kupatikana kwa taarifa za kina za uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi ikiwa ni pamoja na vitabu vya mahesabu vilivyokaguliwa kwa njia na michakato ya kitaalamu na si kubahatisha.