Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela Meatu Simiyu amekamatwa akijipanga kuelekea Moru ndani ya hifadhi ya Serengeti akiwa na malengo ya kwenda kufanya mauaji kwa wanyama aina ya Faru.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amethibitisha kukamatwa kijana huyo na kusema kuwa wamemkuta akiwa na risasi 356, magazine 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha.

Kufuatia kufanikisha kumkamata kijana huyo kabla ya kutekeleza ujangili Waziri Kigwangalla amesema kuwa wataendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za kiintelinjesia kuthibiti ujangili na kudai kuwa watahakikisha wanakamata majangili kabla ya hawajafanya ujangili.

“Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini tumekusudia kukamatas majangili kabla hawajafanya ujangili” amesema Kigwangalla.

Amesema wataisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ys biashara halamu ya ujangili nchini.