Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba 1, 2017 imeifuta kesi ya shambulio inayomkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Kigoma Malima na dereva wake Ramadhani Mohammed Kigwande baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), kuwasilisha Nolle Prosequi.
Uamuzi wa kufutwa na kuachiwa kwa washtakiwa hao umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba ifutwe chini ya kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa Mashauri ya Jinai kufuatia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.
Baada ya wakili Kishenyi kuwasilisha ombi hilo mahakamani hapo Hakimu Mwijage alimuhoji kama anasababu na kwamba kama hana haifuti. Kishenyi alisoma kifungu hicho ambacho kinampa mamlaka DPP kuiondoa kesi mahakamani wakati wowote pale anapoona inafaa na pia kinamruhusu kuirudisha mahakama pia.
Baada ya Kishenyi kukisoma kifungu hicho, Hakimu Mwijage alikubali na kuwaachia huru washtakiwa wote. Kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya shahidi wa pili wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wake.
Hata hivyo, washtakiwa hao walikwishasomewa melezo ya awali (PH), ambapo wote wawili walikubali maelezo yao binafsi, siku ya tukio walikuwepo Masaki, walikamatwa na kushtakiwa na wakayakana mashtaka yote yanayowakabili.

Katika kesi hiyo, Malima anadaiwa kuwa Mei 15,2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi alimzuia ofisa wa polisi H.7818 PC ABDU kufanya kazi yake kwa kumzuia afisa huyo kufanya kazi yake ya kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita Joseph.

Mshtakiwa Ramadhani Kigwande naye anadaiwa, kumshambulia Mwita Joseph kufanya kazi yake, Mwita ni afisa oparesheni wa kampuni ya Priscane Business Enterprises wakati alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari namba T 587 DDL alimshambulia na kumsababishia