Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile amewataka Mfuko wa taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) kuhakikisha watanzania wote wanapaya huduma ya bima ili kuweza kupata matibabu kwa urahisi na wakati sahihi.

Hayo yamesemwa leo alipotembelea makao makuu ya mfuko huo na kujionea namna wanavyofaya kazi zao ikiwemo kuhifadhi nyaraka za madai kutoka katika vituo tofauti vya afya.

Dr Ndungulile amesema, NHIF wanatakiwa kujitanua zaidi ikiwemo kujitangaza na amewasifu kwa huduma nzuri wanazozitoa kwa wananchi pamoja na kutoa vifaa tiba kwa wateja wao.

“napenda niwapongeze NHIF kwa hatua kubwa mliyofikia ya kutoa huduma kwa watanzania na nimesikia kutoka kwa mkurugenzi kuwa mpaka sasa mna asilimia 31 ya watanzania wote lakini mikakati yenu ni kufika asilimia 50 kwa mwaka 2020,”amesema Dr Ndungulile.

Ameongezea katika kuhakikisha wateja wanapata huduma nzuri basi yale malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vituo vya afya kucheleweshewa malipo yao asingependa ayasikie tena, wanatakiwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa wakati na kuwalipa kile wanachostahili.

Naye Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga amesema kuwa wao kama mfuko wa bima kwa sasa wanatoa huduma katika vituo vingi vya afya na pia wameweza kupata idadi kubwa ya wateja wapya.

Konga amesema kuwa, kwa sasa NHIF wanatoa huduma za matibabu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kutoa vifaa tiba, kusafishwa kwa figo, upasuaji na mengineyo.
Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akipata maelezo ya namna Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanavyohifadhi nyaraka zao katika makabati maalumu na yanaweza kudumu kwa zaidi ya miaka saba, Kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga
Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga akimuelezea Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile mikakati yao ilikoanzia na mpaka walipo sasa kwenye utoaji wa huduma za kiafya, pia katika kuendeleza kutoa huduma bora kwa wateja wao ikiwemo kuongezeka kwa wateja wa huduma ya bima kufikia aailimia 50 ya watanzania kwa mwaka 2020.

Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akielezewa jinsi wanavyoweza kushughulikia simu zote za wateja wanazopiga kwa ajili ya kupata huduma, na wanapata takribani simu 200 kwa siku kutoka kwa wateja tofauti kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga

Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Utafiti wa Mfuko wa taifa ya Bima ya Afya Angela Mziray akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine NdungulileNaibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akiwa ametembelea sehemu mbalimbali wakati alipotembelea makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bma ya Afya (NHIF) leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akiwa anasaini katika kitabu cha wageni.

Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akiwa anazungumza na wafanyakazi wa kanda ya Dar es salaam leo wakati alipotembelea makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bma ya Afya (NHIF) na kuwataka waendelee kuitangaza vyema mfuko huo na waje kufikia malengo waliyoyapanga.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga akikambidhi kijarida chenye maelezo yahusuyo Mfuko wa taifa wa bima ya Afya kwa Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile alipotembelea makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bma ya Afya (NHIF) na kuzungumza na wafanyakazi wa mfuko huo kutoka kanda ya Dar es Salaam leo.

Kaimu Mweenyekiti wa Chama cha wafanyakazi Rose Gabriel akitoa neno la Shukrani kwa Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile wakati alipotembelea makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bma ya Afya (NHIF) na kuzungumza na wafanyakazi wa mfuko huo kutoka kanda ya Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bma ya Afya (NHIF) leo Jijini Dar es Salaam.Picha Zote na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.