Mkuu wa mkoa wa dar es salaam PAUL MAKONDA leo amezindua ujenzi wa ofisi za walimu kwa lengo la kuwaboreshea mazingira mazuri ya kufundishia wanafunzi na kufanya kazi katika mazingira mazuri.

Akizungumza  na Wananchi leo katika uzinduzi huo uliofanyika  shule ya Msingi Kichangani iliyopo Majohe MAKONDA amesema ujenzi wa ofisi hizo ni jambo zuri kwani Walimu ni watu muhimu na wanafundisha watoto ila imekua changamoto kwao kwa kukosa Ofisi.

Aidha  Ofisi hizo  zitakapo jengwa zitasaidia katika kutatua changamoto zinazowakabili walimu katika utendaji wa kazi zao, hali ambayo inaweza kusababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

“Nafurahi kuona ujenzi umeanza tena kwa kasi nzurii lakini ujenzi  huu ukikamilika  vifaa vitavyobaki tutatumia  katika kujenga ofisi za shule ya msingi majohe iliyopo karibu na shule hii” Amesema.

Katika hatua nyingine Mkuu wa  wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA amempongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam kwa jitihada zake katika kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira mazuri ili kuweza kutoa elimu bora na ufaulu mzuri kwa wanafunzi.

Hata hivyo Makonda amesema kuna watu wapo Marekani kupitia vyombo vya habari wamesikia zoezi hili la ujenzi wa Ofisi za Walimu hivyo wamejitolea Kontena 12 la vifaa vya ofisini kuanzia viti na kila kitu.