Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kuhusu aina ya vitabu vinavyotumika kufundishia Elimu ya Watu Wazima kutoka kwa Mratibu wa Progaramu ya Elimu Changamano nje ya mfumo rasmi Dkt. Sempeho Siafu kutoka katika Taasisi ya Elimu

Naibu Mkurugenzi Utafiti na Ushauri Dkt. Kassimu Nihuka akifafanulia Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha matumizi ya mashine za uchapaji zilizopo katika karakana ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiangalia baadhi ya mitambo inayotumika kuandaa vipindi vya elimu kwa umma katika studio zilizoko Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

………………

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Ole Nasha ameitaka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kimuundo badala ya kufikiria kufanya miradi ambayo imekuwa ikiwaondoa kwenye mwelekeo wa malengo ya uanzishwaji wa Taasisi hiyo.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea Taasisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuzitambua taasisi zilizo chini ya wizara pamoja na utendaji wa majukumu yake.

Akiwa katika Taasi hiyo amesema nchi bado inaihitaji Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima pamoja na aina ya elimu ambayo inatolewa na taasisi hiyo, hivyo ameitaka taasisi hiyo kutekeleza majukumu yake iendane na hali halisi ya mazingira ya elimu.

Ole Nasha mesema
ukiangalia utekelezaji wa miradi hiyo inabaki kuitwa elimu ya watu wazima lakini namna inavyoendeshwa haziakisi uhalisia wake na badala yake zinabaki kuwa kama mifumo mingine ya utoaji wa elimu ya mfumo rasmi.

Naibu Waziri Ole Nasha akiwa katika taasisi hiyo amepata fursa ya kutembelea chumba cha Uchapaji vitabu majarida, Karakana, Maktaba na idara ya Elimu ya masafa na Studio za kuandaa vipindi vya kuelimisha umma vya Elimu ya Watu Wazima.

Aidha, Naibu Waziri ametembelea Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Elimu, Habari, utamaduni ya UNESCO na kuwataka kuitisha kikao cha wadau wanaohusika na Tume hiyo ili kuzungumzia changamoto za kimfumo na muundo zinazoikabili taasisi hiyo.

Imeandaliwa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizar ya Elimu, Sayansi na Teknolojia