Watu nane wamefariki dunia na wengine zaidi ya 12 wamejeruhiwa kwa kugongwa na na gari katika eneo la Manhattan mjini New York Jumanne hii.

Picha ya gari lililosababisha ajali mjini New York
Meya wa mji huo Bill De Blasio amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiongez kuwa miongoni mwa watyu ambao wamefariki ni waendesha baiskeli.

Inadaiwa kuwa dereva wa gari hilo dogo la mizigo ambalo limesababisha ajali hiyo ni kijana mwenye umri wa miaka 29 ambaye alitoka na bastola mbili kwenye gari hilo baada ya kutokea kwa tukio hilo lakini polisi walimuwahi kwa kumshambulia kwa risasi na kumjeruhi.

Picha ya dereva wa gari lililosababisha ajiali akiwa ameshika bastola mbili
Baada ya kutokea kwa tukio hilo Rais wa Marekani, Donald Trump kupitia mtdandao wake wa Twitter ameandika, “In NYC, looks like another attack by a very sick and deranged person. Law enforcement is following this closely. NOT IN THE U.S.A.!.”
Wakati huo huo vyombo vya habari nchini humo vimenakiri taarifa za polisi kuwa, kijana huyo aliamua kuendesha gari hilo katika njia ya waendesha baisikeli iliyoko eneo la Mto Hudson sehemu ya Lower Manhattan kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi ili kuzuia shambulio alilolipanga.