Picha ya mshitakiwa Sayfullo Saipov

Waendesha mashtaka mjini New York wamefungua mashtaka dhidi ya mhamiaji kutoka nchini Uzbek anayedaiwa kuhusika katika shambulio la gari dogo la mizigo lilitokea jana na kuua watu nane katika mji wa New York nchini Marekani.

Sayfullo Saipov anakabiliwa na mashtaka ya kusaidia kutoa vifaa kwa kundi la kigaidi la Islamic State.

Akizungumzia mashataka yaliyofunguliwa kaimu mwanasheria mkuu JOON Kim amesema Saipov amefunguliwa mashitaka ya makosa mawili ya ugaidi.

Shitaka la kwanza ni kutoa vifa vya kusaidia maandalizi ya shambulio la kigaidi kwa kundi la IS, na shitaka la pili kusababisha uharibifu wa magari ambayo yalisabisha vifo na majeruhi.

Pia Rais Donald Trump amesema anachukua hatua za haraka dhidi ya mfumo wa uhamiaji nchini humo na ametaka adhabu kali kutolewa dhidi ya watu wanaobainika kujihusisha na vitendo vya kigaidi kama hili la New York.

                                        Eneo ambalo shambulizi lilifanyika