Mrembo anayefanya vizuri kwenye anga ya Bongo Fleva, Nandy amewataka watu wanaomfananisha na mwanamuziki mwenzake Ruby kuacha mara moja kwa kuwa kila mtu ana ladha yake ya Muziki.

Akipiga stori na Showbiz Xtra, Nandy amesema, kwa muda mrefu mashabiki wake wamekuwa wakifananisha muziki wake na wa Ruby kitu ambacho haoni kama kina mashiko kwa kuwa kila mtu ana ladha yake ya kipekee ambayo mwenzake kakosa.

“Namheshimu Ruby ni mwimbaji mzuri, lakini kunifananisha naye ni kuukosea heshima muziki wangu, ladha ya muziki wangu ni tofauti kabisa na Ruby kama unaujua vizuri muziki utabaini muziki wetu ni tofauti kabisa,” alisema Nandy bila kufafanua kwa undani zaidi.